Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, September 2, 2013

Wabunge wagawanyika kuhusu Syria

waandamanaji wanaopinga serikali ya Syria.
Wabunge wa Marekani bado hawajafikia maelewano  kupiga  kura juu ya kuunga mkono mashambulizi ya kijeshi dhidi ya serikali ya rais Bashar al-Assad au kupinga. Baadhi yao walizungumza baada ya kupokea taarifa  kuhusu Syria kutoka kwa maafisa wa Marekani Jumapili.

Wanatarajiwa kurejea bungeni Septemba 9 lakini baadhi yao walihudhuria kikao Jumapili jijini Washington ambapo maafisa waliwaelezea mpango wa kuingilia kati mzozo wa Syria. Baada ya kikao hicho baadhi yao walisema wanaamini silaha za kemikali zilitumiwa lakini kungali na maswali kadha.

Mbunge wa chama cha Demokrat Janice Hahn, anauliza ikiwa hii ni sababu ya kwenda vitani. Kuna lengo gani la kwenda vitani? Je tunampa idhini  ya aina gani rais? aliuliza mbunge huyo.

Hahn anasema Marekani haipaswi kuingia vitani peke yake. Naye mbunge wa chama cha Republican Scott Rigell alisifu uamuzi wa rais Obama wa kuomba idhini ya wabunge. Lakini akasema kwa sasa jibu litakuwa ’hapana’. Alisema hataunga mkono kura hiyo kwa sababu haijabainika wazi lengo la kuingia vitani huko Syria ni lipi. Mbunge wa chama cha democrat Sandy Levin anaunga mkono majeshi ya Marekani kuingilia kati mzozo wa Syria. Anasema ana imani kuwa wabunge wataunga mkono kura hiyo kwa sababu wasipofanya hivyo watakuwa wanapeleka ujumbe usio sahihi.

Jumamosi rais Obama alisema hahitaji idhini ya bunge kushambulia, lakini anahitaji uungaji mkono wa wawakilishi wa taifa waliopo Washington.

Jumapili waziri wa mambo ya nje John Kerry alizungumza kwenye vituo kadha vya televisheni akieleza kile ambacho utawala wa Obama umefahamu kutoka na mashambulizi ya mwezi jana  dhidi ya raia mjini Damascus na maeneo jirani. Kerry alisema Marekani isipochukua hatua  itakuwa inampa nafasi dikteta katili kuendelea kutumia gesi ya sumu dhidi ya watu wake.
Imewekwa na Happy Adam
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment