Writen by
sadataley
2:47 PM
-
0
Comments
Mahakama nchini India imewahukumu wanaume wote wanne kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumuua mwanamke katika basi katika mji mkuu wa India Delhi mwezi Desemba mwaka jana.
Mmoja wao aliangua kilio na kuanguka baada ya kutangazwa kwa hukumu dhidi yao .
Karibu miezi 9 baada ya ubakaji ulioitikisa India, jaji ametoa hukumu kwa wanaume wote wanne ambao tayari walikuwa wamepatikana na hatia ya uhalifu .Msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23 aliumizwa sana na baada ya wiki moja alifariki kutokana na majeraha .
Wendesha mashtaka walikuwa wamewaombea hukumu ya kifo wakisema ingetoa ishara muhimu kwamba uhalifu wa aina hiyo hautakubalika kamwe .
Familia ya mwanamke huyo pia waliomba wanaume hao wanyongwe .
Lakini mawakili watetezi wa wanaume hao walipinga mapendekezo ya hukumu ya kifo , wakisema wateja wao hawakuwa na rekodi za uhalifu awali na kwamba wanastahili kusamehewa .
Kifo cha mwanafunzi huyo mwezi Disemba mwaka jana kilisababisha maandamano makubwa ya upinzani kote nchini India , yaliyoilazimisha serikali kubadili sheria zilizokuwepo za uhalifu wa ngono
No comments
Post a Comment