Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, September 11, 2013

Ugunduzi wa maji kenya waleta afueni

Eneo la Turkana linakabiliwa na uhaba wa maji sana
Serikali ya Kenya imetangaza ugunduzi wa visima vikubwa vya maji chini ya ardhi ambavyo vinaweza kumudu mahitaji ya maji katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini ijayo katika jimbo la Turkana na kwa nchi nzima.
Visima hivyo bila shaka vitaleta afueni kwa wakaazi kwani Turkana ni eneo kame Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Eneo hilo pia lina viwango vya juu vya umaskini.
Ugunduzi huo ulitokana na utafiti wa wanasayansi waliotumia teknolojia ya satellite
Visima hivyo vinapata maji kutoka kwa chemichemi za maji kutoka milima ya mbali kwa hivyo maji yake yakitumiwa vyema huenda havitawahi kukauka.
Mamilioni ya wakenya wanakosa maji safi.
Nchi hiyo pia inakabiliwa na msimu tata wa mvua na inakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Utafiti ulifanywa na shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO na wanasayansi wa Kenya kwa ufadhili wa serikali ya Japan.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment