Writen by
sadataley
12:30 PM
-
0
Comments
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaja makubaliano kati ya Marekani na Urusi kuhusu silaha za kemikali za Syria kama hatua muhimu katika suluhu kubwa zaidi la mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo.
Lakini kwenye hotuba yake bwana Hollande aliongeza kusema kuwa "lazima wazo la kuchukulia Syria hatua za kijeshi lisalie , la sivyo hapatakuwa na shinikizo.’’
Aidha Bwana Hollande alisema huenda nchi wanachama wa baraza hilo wakakubaliana kuhusu kura katika baraza la usalama la umoja wa Mataifa kwa azimio kuhusu Syria.
Holland anatarajiwa kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry hii leo kujadili swala hilo.
Rais huyo amesema kuwa sharti Syria iwekewe vikwazo ili iharibu silaha zake za kemikali ikiwa itakataa kufuata maagizo na matakwa ya mataifa ya nchi za kigeni.
"Ni muhimu kuongeza kwa haya yote tisho la kuiwekea Syria vikwazo ikiwa makubaliano na malengo ya baraza la usalama ya Umoja wa Mataifa hayatatimizwa,’’ aliongeza kusema Rais Hollande
"Lakini hatua inayofuata ni kutafuta suluhu la kisiasa kwa haya yote.’’
No comments
Post a Comment