Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, September 15, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kila mmoja wetu anajua kwamba leo ni siku ya Democrasia duniani inamaana mtu yoyote au Taasisi inayouhuru wa kutoa maoni juu ya jambo hili katika taaifa lolote lenye kufuata misingi ya utawalabora kwa misingi ya Demokrasia
Mataifa yote ulimwenguni yanaadhimisha siku hii muhimu kwao ambayo uwepo huu wa Democrasia umekuwa ni chachu ya maendeleo makubwa ndani ya nchi na rai wao.
Katika Nchi yenye kufuata msingi wa Demokrasia mtu na taasisi hutoa maoni yao waliyonayo kwa mustakabali wa nchi katika kuwa na utawala wa haki na sheria .
Linaloshangaza wengi, tokea kuanzishwa mfumo wa vyama vingi hapa kwetu Zanzibar mnamo mwaka 1992 hadi leo hii niwazi kabisa kuwa mfumo huu wa Democrasia bado unayumbishwa na baadhi ya watu kwa maksudi bila kujali thamani ya Taifa.
Hii inamaana Zanzibar bado inasuasua kuufuta utaratibu huu bora katika kutawala na kuongoza Nchi na hatiame kuwa miongoni mwa mataifa yanayotupiwa sifa ulimwenguni kwa ufuataji bora wa mfumo huu,ili kuweza kuiletea maendeleo nchi yetu kama zilivo nchi nyengine Duniani kote.
Ni wazi kabisa kuwa ndani ya Zanzibar Democrasia hairidhishi kwani hadi leo kunanjama za maksudi kuwanyima Wazanzibar vitambulisho vya uzanzibar mkaazi kwa lengo tu lakuwafanya wasiweze kupiga kura na hatimae kupunguza idadi ya wapiga kura katika chaguzi mbalimbali.
Ni dhahir tena kwa makusudi serikali kupitia masheha wake wamekuwa wakiwakwamisha baadhi ya watu kupata haki zao nyingi ikiwemo vitambulisho hivyo kwa kisingizio cha kisiasa, hivi nikweli tutafika kwa kufuata mwenendo huu?
Kila mmoja anaelewa kwamba hivi sasa Tanzania imo katika mchakato wa kuandika katiba mpya, kunasheria mbalimbali zimefanyiwa mabadiliko bila ya raia kushirikishwa halafu kiongozi mmoja tu wa Serikali kwa maslahi yake anathubutu kusimama mbele ya bunge kwamba Zanzibar imeshirikishwa kikamilifu katika kuifanyia mabadiliko sheria ya mabadiliko ya katiba hiyo.
Lakini kiongozi huyo alisutwa na baadhi ya Taasisi hapa Visiwani Zanzibar baada ya kusema bila kificho kwamba wao hawakushirikishwa katika kuiboresha sheria hiyo.
Katika kuthibitisha kwamba Demokrasia bado Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania likipitisha muswaada wa kufanyiwa marekebisho sheria ya katiba huku Wabunge wote wa vyama vya upinzani wakikataa kata kata na hatimae kutoka nje kabisa kwa kutokuridhika na utaratibu mzima wa maboresho ya sheria hiyo.
Kwa kutokushirikishwa kwa wazanzibar na kunyimwa haki yao ya Kidemokrasia katika mchakato wa kuitolea maoni sheria hiyo katika kuelekea kuwa na katiba mpya Tanzania ni wazi kwamba bado demokrasia inayumba.
Kilichofanyika ni kuwepo kwa barua za viongozi watatu na maoni ya vyama viwili kwa mujibu wa Naibu Spika wa Bunge kwa sehemu hizo tano zinawasemea wanzanzibar wapatao 1300,000, kutokana na hali hiyo ni wazi kwamba bado Demokrasia inasuasua hapa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Ndani ya Baraza la Wawakilishi kwa upande wa Zanzibar huunda kamati kamati mbalimbali kama ilivyo Bunge la Jamuhri kwa lengo kuangalia mwenendo pamoja na matumizi ya mali za Umma.
Kamati hizo zimekuwa zikigundua ubadhirifu mkubwa katika Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuazia watendaji hadi Mawaziri wa serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi bila kuchukuliwa hatua yoyote na kiongozi mkuu wa taifa hili changa.
Hawa wote hawachukuliwi hatua kwa sababu bado Zanzibar haijataka kufuata misingi bora ya utawala wa Kidemokrasia ambayo ndani hupata utawala bora wenye misingi ya haki na sheria.
Kutokana na hayo yote tuliyoyaona ni makosa ambayo yanaweza kurekebishwa bila vikwazo kwenye nia njema ya Nchi, Chama cha wananchi CUF kinatoa ombi kwa Taasisi au viongozi wote wenye nafasi kubwa kuendesha shuhuli zao kwa kufuata misingi ya Demokrasia ili kila raia aweze kupata haki yake.
Ni vyema kuangalia maendeleo yaliopatikana katika mataifa yanayofuata mfumo wa Demokrasia na si vibaya na Zanzibar ikafuata nyao zao ili kufikia maendeleo na umoja.
Tunawatakieni siku njema ya maadhimisho ya siku ya Democrasia Duniani kote na matumaini yetu Zanzibar itatumia siku hii kujipima na kujirekebisha ili kufikia katika kiwango bora cha kufuata mfumo huo.
‘’HAKI SAWA KWA WOTE’’
Mkurugenzi wa haki za Binaadamu, Habari, Uenezi, Mahusiano na Umma (CUF)
Salim Bimani
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment