Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, September 11, 2013

Obama aunga mkono diplomasia Syria lakini shambulizi la kijeshi bado lawezekana.

Obama akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni kuhusu maamuzi yake huko Syria.
Obama akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni kuhusu maamuzi yake huko Syria.
Rais Obama ameeleza mpango wake wa kuzuia serikali ya Syria kutumia silaha za kemikali  jumanne na rais aliunga mkono kwa tahadhari pendekezo la Russia  kutanzua mzozo huo.
Obama amesema shambulizi la Marekani huko Syria litakuwa lenye malengo maalum katika kuharibu matumizi ya kemikali.
Rais amesema hatapeleka wanajeshi  wa Marekani  huko Syria na hatafanya operesheni isiyojulikana  mwisho wake kama vile Iraq na Afghanistan  na mashambulizi ya ndege ya muda mrefu kama ilivyokuwa Libya au Kossovo.
Amesema anajua hali mbaya ya vifo viliyosababishwa na vita vya Iraq na Afghanistan , kwamba wazo lolote  la  vita halitapendwa na watu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment