Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, September 17, 2013

Mwanasiasa kunyongwa Bangladesh

Mahakama ya Juu nchini Bangladesh imemhukumu kifo kiongozi wa kiisilamu aliyepatikana na hatia ya mauaji ya halaiki wakati wa vita vya Ukombozi kutoka kwa Pakistan mwaka 1971.
Abdul Quader Mollah
Mahakama hiyo ilikataa rufaa yake dhidi ya hukumu ya maisha jela na kumuhukumu kifo kwa makosa ya jinai.
Abdul Quader Mollah wa chama cha upinzani cha Jamaat E Islami alihukumiwa maisha na mahakama maalum ya uhalifu wa kivita hapo mwezi Fabruari.
Wakili wake amesema hii ndio mara ya kwanza hukumu ya maisha imeongezwa na kua kunyongwa.
Hukumu ya awali ilichochea maandamano ya wafuasi wa chama chake ambao wamesema hukumu dhidi ya Mollah imechochewa kisiasa.
Lakini wapinzani wake wanasema kuwa hukumu hiyo ni dhaifu mno.
Maelfu walifanya maandamano kote nchini wakitaka Mullah ambaye alipatikana na hatia ya kuongoza mauaji ya halaiki wakati wa vita vibaya zaidi vya kupigania uhuru anyongwe.
Maandamano hayo yalichochea bunge kufanya mageuzi ya sheria ambayo yanaruhusu serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wowote ulioafikiwa na mahakama maalum ya uhalifu wa kivita nchini humo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment