Writen by
sadataley
9:58 PM
-
0
Comments
Polisi mjini Washington wamethibitisha kuuawa kwa 'watu kadhaa' katika shambulio la risasi katika makao makuu ya jeshi la wanamaji mjini humo.
Watu wengine 4 - akiwemo afisa wa polisi wamejruhiwa vibaya, maafisa wamesema.
Polisi waliingia jengo hilo wakimsaka mshambuliaji baada ya risasi kuripotiwa kusikika asubuhi. (13:20 GMT).
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi mjini Washington, Cathy Lanier, Mshambuliaji mmoja aliuawa papo hapo na polisi bado wanawasaka wengine wawili wanaoaminika kuhusika.
Afisa mmoja wa idara ya Ulinzi ya wanamaji ya Marekani, mwenye umri wa miaka 50- ametambuliwa kama aliyeuawa kwa mujibu wa taarifa katika shirika la habari la ABC.
Polisi sasa wanasaka eneo linalozunguka makao hayo ya kijeshi.
Bi Cathy amesema, '' Wasiwasi wetu mkubwa kwa sasa ni kuwa tumebakia na washambuliaji wengine wawili na hatujui waliko.''
Alisema kuwa mmoja wao alikuwa amevalia shati lenye mikono mifupi, mshono wa kijeshi na kofia la kijeshi. Alionekana mara ya mwisho akiwa amebeba bunduki mkononi.
Mshukiwa mwingine ni mweusi mwenye umri wa miaka 50 , ambaye pia amebeba silaha mkononi.
Taarifa ya Ikulu
Rais Barack Obama amepewa ripoti kamili na maafisa wakuu na ameagiza vyombo vyote vya uchunguzi kushirikiana katika uchunguzi huo.
Akizungumza katika ikulu ya White house, bwana Obama amesema anahuzunishwa na tukio lingine la mauaji ya watu wengi katika ardhi ya Marekani. Ametoa rambi rambi zake kwa familia za waathiriwa.
"Hawa ni wake na waume walioamka kwenda kazini kama kawaida'' Alisema. '' Ndio wanafahamu kuwa wanakabiliwa na hatari wakiwa oparesheni kule nje. Lakini leo wamekumbwa na uhasama mbaya wasiotarajia wakiwa nyumbani.''
zaidi ya watu 3,000 wanafanya kazi katika jumba hilo ambalo ndilo makau makuu ya kutengeneza silaha, kununua silaha na pia kutoa huduma za kila siku kwa manuari za kivita za Marekani.
No comments
Post a Comment