Writen by
sadataley
10:41 PM
-
0
Comments
Sura yake kabla ya shambulio. |
Padri huyo ambaye leo hii alitembelewa na Rais wa Zanzibar, Dk Shein, alionekana kuzungumzia hali ilivyokuwa tete visiwani humo na kumwambia Rais kuwa hata wageni wanamwagiwa tindikali (akizungumzia mabinti wawili kutoka Uingereza), na kisha kumwambia "this is too much". Ambapo Rais Shein alimhakikishia kuwa watawafuatilia walihusika na tukio hilo, na baada ya kusikia hivyo, Padri anamshukuru Rais. Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) imeripoti kwenye taarifa yake ya habari saa mbili usiku.
Katika kufuatilia mwendelezo wa taarifa hizi, Gospel Kitaa imefahamu kuwa Padri Mwang'amba amehamishiwa jijini Dar es Salaam kwenye hospitali ya Muhimbili aktiokea hospitali kuu ya Mnazi Mmoja visiwani humo, kutokana na hali yake ya afya kutoridhisha na hivyo kuhitaji matibabu zaidi.
Rais Shein amelitaka jeshi la polisi kufuatilia ipasavyo na kuhakikisha wanatokomeza vitendo hivyo ambavyo havivumiliki na pia ambavyo vinaitia serikali hiyo aibu ndani na nje ya nchi mipaka yake.
Padri Anselmo Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae alimwagiwa tindikali siku ya Ijumaa alasiri, akitoka kwenye 'Internet Café' maeneo ya Mlandege.
Vitendo hivi si vya kuchekelea hata kidogo, na kama serikali isipotilia mkazo na kuchimbua vyanzo vya mashambulizi ya namna hii, basi wananchi hawatokuwa na furaha popote walipo kwenye nchi hii huru, isiyo na dini wala kabila - bali umoja wa Tanzania. Vinginevyo itabatizwa jina - kuwa ni nchi ya tindikali na madawa ya kulevya badala ya lile jina zuri tulilozoea, kisiwa cha amani.
TAHADHARI: Picha ifuatayo sio nzuri kuonwa na kila mtu hasahasa kwa watu wenye hisia kali, kwa kubonyeza hapo chini, (Endelea Kusoma) basi utatafsiriwa kuwa umejiandaa kisaikolojia kuitazama.
TAHADHARI: Picha ifuatayo sio nzuri kuonwa na kila mtu hasahasa kwa watu wenye hisia kali, kwa kubonyeza hapo chini, (Endelea Kusoma) basi utatafsiriwa kuwa umejiandaa kisaikolojia kuitazama.
Padri Anselmo Mwang'amba akiwa hospitalini. ©Martin Kabemba/Sophie Mbeyu Blog |
No comments
Post a Comment