Writen by
sadataley
12:42 PM
-
0
Comments
Na Masoud Masasi, Mwananchi
Dodoma.Waziriwa Viwanda, Biashara na Masoko, Abdallah Kigoda amewataka wazalishaji asali nchini kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao hilo kwa kuwa mahitaji yake katika soko la ndani na nje ya nchi yameongezeka.
Waziri huyo ameyasema hayo juzi mjini hapa alipokuwa akizinduzia mradi wa ufatiliki wa zao la asali nchini ulioandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya GS1 Tanzania.
Kigoda alisema mahitaji ya asali katika soko la nje ni makubwa kuliko uwezo wa uzalishaji nchini ambao ni wa asilimia 25 pekee huku wazalishaji hao wakihimizwa kufanya kazi ya ziada kuongeza uzalishaji ili uende sambamba na soko la zao hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu alisema lengo la mradi huo ni kuanzisha na kuendeleza ufugaji wa kisasa wa nyuki unaozingatia utunzaji wa mazingira ili kuongeza uchumi na kipato cha wafugaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania, Fatma Kange alisema wameanza na mikoa 10 katika mradi huo ambayo ni Morogoro, Dodoma, Pwani, Tanga, Manyara, Kigoma, Singida na Katavi.
No comments
Post a Comment