Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, September 14, 2013

Azimio halitataja hatua ya kijeshi Syria

Marekani inaonesha kuwa iko tayari kuacha kutaja hatua ya kijeshi katika azimio lolote la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria.
Ban Ki Moon, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Maafisa wa ikulu ya Marekani walisema kumepatikana maendeleo katika juhudi za kupata azimio linalokubalika, ambalo linaweza kujadiliwa baada ya ujumbe wa wakaguzi wa silaha za kemikali wa Umoja wa Mataifa kutoa ripoti yao Jumatatu.
Mazungumzo baina ya Marekani na Urusi kuhusu namna ya kudhibiti shehena ya silaha za kemikali za Syria yanaendelea kwa siku ya tatu.
Huku nyuma, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-Moon, anasema anataraji kutafanywa duru ya pili ya mazungumzo ya amani kuhusu Syria, mwezi ujao.
Akizungumza kwenye televisheni ya Ufaransa, Bwana Ban alisema amezungumza na mjumbe wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu, Lakhdar Brahimi kuhusu swala hilo hapo Ijumaa na wote wawili wanaona hilo ni jambo muhimu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment