Writen by
sadataley
9:18 PM
-
0
Comments
Imeandikwa na Immaculate Makilika; video na IKULU — RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ametunuku Hati Idhini ((University Charter)) kwa vyuo vikuu na vyuo vishiriki 8 baada ya vyuo hivyo kutimiza taratibu zote za uanzishwaji wake hapa nchini.
Vyuo vilivyotunukiwa hati baada ya kutimiza taratibu zote ni Chuo Kikuu cha Tumaini (TUMA), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (RUCo), Chuo Kikuu cha Mount Meru (MMU), pamoja na Chuo Kikuu cha Arusha (UoA).
Vyuo vingine vilivyotunukiwa hati hiyo ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo), Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia Arusha (NM-AIST) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
Rais Kikwete alivitunuku vyuo hivyo kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo
alisema vimepiga hatua kubwa ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiandikisha hadi kufikia laki moja sitini na sita elfu mwaka 2013, ukilinganisha na idadi ya wanafunzi elfu arobaini ya mwaka 2005.
“Idadi kubwa ya wanafunzi pekee haitoshi,ubora wa elimu uzingatiwe . Ikiwemo kupata wakufunzi wengi na wenye sifa ni lazima sisi wenyewe tuwekeze ndani ili kupata wakufunzi wakutosha katika vyuo vyetu,” alisema Rais Kikwete.
Aidha Rais Kikwete alivitaka vyuo hivyo kutekeleza mkakati wa elimu wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) ipasavyo ili kuboresha elimu nchini kwa kuimarisha miundombinu ya vyuo vikuu nchini.
Aliongeza kuwa lazima viwe na mahitaji yote muhimu kwa kutoa elimu bora ikiwemo vifaa vya kutosha, maabara, vyuo vya zamani viwekwe kwenye viwango ili kukidhi utoaji wa elimu bora, na kusisitiza vyuo vikuu vyetu vishirikiane na vyuo vikuu vya nje na kuvishauri vitafute vyanzo vingine vya mapato ili kukidhi uendeshaji badala ya kutegemea ada.
Utoaji wa Hati Idhini kwa vyuo vikuu ni zoezi endelevu linalolenga kuboresha kiwango cha utoaji elimu ya juu nchini ili kuwezesha wahitimu kukabiliana na changamoto za maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.
Mara ya mwisho zoezi hili lilifanyika tarehe 18 Agosti, 2010 ambapo jumla ya vyuo vikuu na vyuo vishiriki 13 vilitunukiwa Hati Idhini.

No comments
Post a Comment