Writen by
sadataley
9:32 AM
-
0
Comments
Igunga. Mkuu wa Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora, Elibariki Kingu, amewaasa viongozi wa dini kutokujihusisha na masuala ya siasa, badala yake wajenge misingi ya kiroho kwa waumini.
Akizungumza kwenye tamasha la uzinduzi wa albamu ya nyimbo za Injili ya Anna Nzogi, Kingu alisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakijihusisha na siasa na kuacha kumtumikia Mungu, hali ambayo inaleta vurugu.
Kingu alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia fedha nyingi kufanya mambo yasiyompendeza Mungu, badala ya kuwekeza kwa shughuli mbalimbali za maendeleo na kutoa sadaka na kwamba, watumie uwezo wa Mungu aliowajalia.
No comments
Post a Comment