Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, August 3, 2013

POLISI WAKABIDHIWA GARI LA KUFICHUA UHALIFU


Mku wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali  Said Mwema akitiliana saini hati ya ushirikiano ya kuchunguza uhalifu  baina ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Uturuki na Mkurugenzi wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki Zeki Catalakaya-picha na Issa Michuzi

 Haya huu ni ufunguo tumepewa tayari kazi kwetu sisi sote hapa-picha na Issa Michuzi
SERIKALI ya Tanzania imetangaza kiama kwa wahalifu wote baada ya kukabidhiwa gari maalumu (Crime Scene Van) litakalosaidia kufichua uhalifu unaoendelea nchini. Akizungumza wakati wa kutiliana saini mkataba wa ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Jeshi la Polisi la Uturuki, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, alisema gari hilo litasaidia kutoa ushahidi uliovuka kiwango, ikiwa ni sehemu ya kuondoa dhana potofu.

“Uhalifu sasa basi, kwa kuwa tutahakikisha tunapambana nao kuleta maendeleo kwa kuwa uhalifu ni sehemu moja inayokwamisha maendeleo,” alisema Mwema.

Alisema makabidhiano haya ya gari ni sehemu ya maridhiano baina ya Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Uturuki katika ziara yake ya siku tatu aliyokuja hapa nchini.

Alisema kutokana na kuwapo kwa fursa mbalimbali katika maridhiano hayo, walipata fursa ya kuwa moja ya sehemu inayosaidiwa na Uturuki.

“Tayari askari wetu 21 wamepatiwa mafunzo yanayotokana na jinsi ya kupambana na uhalifu ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi wa kazi zao,” alisema Mwema.

Alisema gari hilo pia litasaidia kuchukua taarifa za uhalifu pamoja na sura ya muhusika wa tukio hilo la uhalifu.

“Kesi nyingi za uhalifu zinaishia njiani kwa sababu ya kukosa ushahidi uliovuka mipaka, hii inatokana na kutoridhika na ushahidi unaotolewa, lakini kwa sababu ya hili gari endapo kama mhalifu atabainika na hatia hana sababu ya kukataa kwa sababu sura yake na taarifa zote tutakuwa nazo,” alisema Mwema.

Alisema watatoa fursa kwa askari wake kwenda Uturuki kujifunza namna jeshi hilo linavyokabiliana na uhalifu ambapo Waturuki watapata fursa ya kuja nchini kujifunza mbinu za kukabiliana na uhalifu.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, alisema ni jambo la faraja kwa Tanzania kupatiwa gari hilo kwa kuwa kwa kiasi kikubwa litasaidia kufichua mambo mbalimbali ya uhalifu.

Alisema itasaidia kubadilishana utaalamu wa kiuchunguzi wa kihalifu unaosababishwa na majambazi ikiwamo kuuwa au kubaka.
http://www.mtanzania.co.tz
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment