Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, August 14, 2013

Maombi ya DPP dhidi ya Abdallah Zombe kusikilizwa Agosti 26 mwaka huu

Dar es Salaam. Maombi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), ya kukata rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wanane yamepangwa kusikilizwa Agosti 26, mwaka huu.
DPP aliwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa yake dhidi ya Zombe na wenzake.
Awali DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru Zombe na wenzake katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva teksi mmoja wa Manzese jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Mei 8, 2013, Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali rufaa hiyo kutoka na kasoro za kisheria zilizobainika katika hati ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa (Notice of Appeal).
Kasoro hiyo iliyobainika kwenye taarifa ya kusudio la kukata rufaa ni kuandika kuwa hukumu inayopingwa ilitolewa na Jaji Salumu Massati wa Mahakama ya Rufani, badala jaji wa Mahakama Kuu.
Hata hivyo mahakama hiyo imetoa fursa nyingine kwa DPP kukata rufaa nje ya muda kwa kuzingatia Sheria ya Ukomo wa Muda.
Kutokana na kupewa upenyo huo wa kurejea tena na rufaa hiyo, DPP alilazimika kuwasilisha maombi Mahakama Kuu akiomba kibali cha kukata rufaa hiyo nje ya muda.
Habari kutoka katika vyanzo vyetu vya Mahakama Kuu zinasema kuwa maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na Jaji Aloyisius Mujuluzi, Agosti 26, mwaka huu.
Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo DPP atatoa hoja au sababu ambazo zitairidhisha mahakama hadi iweze kukubali maombi hayo na kuridhia kumpa kibali cha kukata rufaa hiyo nje ya muda.
Mahakama hiyo inaweza ama kuyakubali au kuyakataa maombi hayo kama haitaridhika na sababu zitakazotolewa na DPP, au kama hakutakuwa au kutakuwa na pingamizi la msingi wa kisheria kutoka kwa upande wa utetezi jambo linalosubiriwa kwa hamu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment