Writen by
sadataley
7:43 AM
-
0
Comments
Wagombea urais,Soumaila Cisse,(Kushoto) na Boubacar Keita, (Kulia)
Kampeni zimekamilika nchini Mali kabla ya uchaguzi wa marudio Jumapili. Wagombea wawili wa kiti cha rais walifuta mikutano ya hadhara Ijumaa kuadhimisha mwisho wa mwezi wa Ramadhan, mwezi mtukufu kwa Waislam.
Mgombea Ibrahimi Boubacar Keita ambaye anaonekana kuwa na na nafasi nzuri katika uchaguzi huu ameahidi kurejesha amani katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo limedumazwa na mapinduzi ya serikali yaliyofanywa na majeshi na wimbi la maasi ya wanamgambo kutoka upande wa kaskazini mwa nchi.
Keita alipata asili mia 40 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi mwezi jana dhidi ya mpinzani wake wa karibu Soumalia Cisse ambaye zamani alikuwa waziri wa fedha.
Cisse alidai kulikuwa na wizi wa kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi lakini amesema atakubali matokeo ya uchaguzi wa Jumapili.
Atakayeshinda uchaguzi huu ana muda wa miezi miwili kuanza mazungumzo na waasi wa Tuareg wanaopigana kujitenga na Mali upande wa kaskazini mwa nchi, kama sehemu ya makubaliano ya sitisho la mapigano na serikali lililofikiwa mwezi Juni.
Imewekwa na Happy Adam
No comments
Post a Comment