Writen by
sadataley
12 years ago
-
0
Comments
Kwaya ya watoto waliokatika malezi maalum kupitia shirika
liitwalo Compasion katika Ushirika wa
Kihesa wamefanikiwa kuzindua albamu yenye nyimbo 9 inayokwenda kwa jina la ‘WAMTUMAINIO
BWANA’.
Uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Chuo
cha Ualimu Kreluu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Wachungaji
wa Kanisa la Kilutheri liliko mjini Iringa.
Katika uzinduzi huo uliofanyika huku mgeni
rasmi akiwa mbunge wa viti maalum Lita Kabati
ulifana kwa kwaya hiyo kuweza kuburudisha kwa nyimbo za kumsifu MUNGU na kuweza
kuwateka mashabiki waliohudhuria
Katika uzinduzi huo Lita Kabati aliweza kuchangia kiasi cha
shilingi milioni 1 albamu hiyo nyimbo za ‘Njooni kwangu, Chagueni,Twashukuru,
Heri,Wamtumainio Bwana unaobeba jina la Albamu, Siendi kwa Shetani, Ninaye
Yesu, Tazama na Baba.
Kwaya hiyo ilifungua na wimbo wa Tushukuru Muumba uliopokelewa vyema na mashabiki na wimbo wa
pili Nitaimba sifa zako kutoka katika albamu ya Wamtumainio Bwana iliyofanywa
na studio za MBC-Hot media ya jijini Dar es salaam.
Wasanii waliosindikiza uzinduzi huo pamoja na Eunice Bujiku
anayetamba na wimbo wake wa ‘Fadhila za
Bwana, Kwaya ya Uinjilisti Kihesa, Kwaya ya Usharika wa
Kihesa, Kwaya ya Vijana-Kihesa na na msanii wa nyimbo za dini anayekuja kasi Atosha Kisava .
Mkuuwa Jimbo la Kaskazini Kihesa Mchungaji Donald Kiwanga
alisema wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi kuwa lengo la kuzindua albamu hiyo ni
kuweza kupata mapato ambayo yataweza kuwasaidia wanakwaya hao kuboresha makazi
yao na matumizi ya Kanisa la MUNGU.
Mpaka mwisho zaidi ya milioni sita zilikuwa zimepatikana
ikiwa ni fedha taslim na ahadi
No comments
Post a Comment