Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, August 24, 2013

FUNGAMANO LA MAKANISA DUNIANI: MADHEHEBU YOTE YANAPASWA KUUNGANA ILI KULETA AMANI NCHINI MISRI

Hayo yamesemwa na Katibu  Mkuu wa Baraza la Fungamano la Makanisa  Duniani (WCC) Mchungaji Dk Olav Fykse Tveit. akielezea juu ya ghasia zilizoko Misri na kutoa  wito kwa madhehebu mbalimbali  kuomba  kwa ajili ya amani na usalama nchini Misri.

Ameyataka madhehebu yote kuwa moyo wa  kufanya kazi pamoja ili kuwaita  wengine wamuone Mungu  kama  ulinzi na kukuza utakatifu wa maisha ya binadamu na maeneo ya kidini.

Akirejea madai yaliyotolewa katika taarifa, Tveit alisisitiza kuwa "hali ya baadaye ya Misri kwa haki na amani inawezekana tu kwa njia ya ahadi ya Wamisri wote."

"Ulinzi wa maisha yote ya binadamu na maeneo takatifu ni jukumu la kawaida la Wakristo na Waislamu. Fungamano la Makanisa  Duniani linasaidia na inasimama katika mshikamano na wito kwa hatua ya pamoja na juhudi kwa ajili ya maridhiano na usalama na viongozi wa dini nchini Misri, "aliongeza.


Katika matukio ya hivi karibuni kufuatia maandamano ya Agosti 14, mamia ya watu wameuawa , wakati Makanisa na Misikiti kadhaa ilichomwa katika  mji mkuu wa Cairo na maeneo mengine.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment