UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Tuesday, August 6, 2013

BAADA YA KUSUKWA UPYA SASA GLORIOUS CELEBRATION YAACHIA NYIMBO MPYA

Baada ya kusukwa vyema kwakundi la Glorious Celebration lenye makao makuu yake Chang'ombe jijini Dar es salaam, hatimaye hapo jana jumapili limeachia nyimbo tatu katika vituo mbalimbali vya radio nchini kwakuanza na zilizopo jijini tayari kuanza kusikika ikiwa ni utangulizi wa album yao mpya.

Akizungumza na GK bwana Lyanga George ambaye ni mmoja wa viongozi wa kundi hilo, ametaja majina ya nyimbo hizo ambazo wamerekodi live ni pamoja na Niinue(ukiwa na mahadhi ya rock au aina ya muziki wa kundi la Hillsong), Wakawaka wenye mahadhi aina tatu ukianza na sebene, reggae na kumalizikia na kwaito na wimbo wa tatu ni Niguse kwa Roho ambao mapigo yake ni ya wastani si haraka wala taratibu mahadhi yakiwa kutoka bondeni, nyimbo zote tatu zikiwa utunzi wake Lyanga huku waimbaji wakiwa tofauti.

Aidha Lyanga amesema album yao hiyo wameanza kuiandaa mapema mwezi wa tatu mwaka huu na inatarajia kuwa na jumla ya nyimbo nane na kwamba ifikapo October mwaka huu watakuwa wameshaachia album nzima ambayo wanafanya chini ya mtayarishaji wa siku nyingi Allan Mapigo na kwamba G.C imejaribu kuangalia mahitaji ya watu kwasasa ndio maana wakaandaa album hiyo ambayo wamesema itakidhi mahitaji yao "Unajua wapenzi wa muziki wa gospel siku hizi sio kama wa enzi zile ambao walikuwa hawachagui aina gani ya nyimbo wanataka kitu ambacho ni tofauti na sasa hivyo unahitajika umakini ambao ndio tumeufanya chini ya Roho Mtakatifu" amesema Lyanga.

Lyanga ameiambia GK kuwa baada ya kuachia album hiyo ndipo wataanza kuandaa video yao ambayo maandalizi yake pia yatatokana na uhitaji wa watu, zaidi amesema maono waliyonayo G.C ni kuona muziki wao unabariki na kuvuta watu wengi kwa Yesu na kwamba wanataka kumtumikia Mungu katika viwango vya juu sana na kutokana na hilo mawazo yao si kuangalia hapa nchini tu bali itakuwa kimataifa. Ambapo kabla mwaka huu haujaisha wanataka kufungua shule ya muziki itakayotumika kufundisha mambo ya muziki kwa watu wote lakini pia wanatarajia kufungua studio ya muziki ya kundi hilo na maandalizi yamekwisha anza.
Habari na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment