Writen by
sadataley
9:08 PM
-
0
Comments
Siku ya jumapili katika usharika wa Kinondoni kanisa la Kilutheri kumefanyika siku maalumu kwa ajili ya kundi la Fellowship ikiwa ni madhumuni ya kusapoti huduma inayofanywa na kundi hilo ambalo linawajumuisha washarika wote ambao hushiriki ibada za jumapili pamoja na katikati ya wiki. Ambapo pia Fellowship hiyo ina kikundi cha kwaya ambayo imekuwa ikibariki waumini wa usharika huo, mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama Allen Mwaipaja akiongozana na Onai Joseph waliweza kuwabariki waumini kwa huduma yao.
Katika kuisindikiza siku hiyo kwaya za Uinjilisti Sayuni, uamsho Amkeni walikuwa sambamba na wenzao hao wa Fellowship katika kuongoza Sifa na kuabudu.
Katika kuisindikiza siku hiyo kwaya za Uinjilisti Sayuni, uamsho Amkeni walikuwa sambamba na wenzao hao wa Fellowship katika kuongoza Sifa na kuabudu.
Waimbaji wa kwaya ya Fellowship wakiwa wamependeza katika sare zao nadhifu. |
Allen Mwaipaja akiimba "Nimeuona mkono wa BWANA" akipata tafu kutoka kwa waimbaji wengine. Chanzo: Blog ya Gospel kitaa |
No comments
Post a Comment