Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Thursday, June 8, 2017

Waingereza milioni 46 kupiga kura leo

London. Mbivu na mbichi za uchaguzi mkuu nchini Uingereza zitajulikana leo baada ya zaidi ya watu 46.9 milioni wa nchi hiyo kupiga kura.

Upigaji kura utaanza saa 1 asubuhi, (saa za Uingereza) wakati ambapo zaidi ya vituo 40,000 vitafunguliwa kote nchini humo.

Katika uchaguzi huo, jumla ya wabunge 650 watapigwa kura.

Idadi hiyo ya wapiga kura 46.9 milioni  ni ongezekao kubwa ukilinganisha na  wapiga kura 46.4 waliojiandikisha mwaka 2015.

Kura nyingine tayari zimepigwa  kwa njia ya posta ambazo zilichukua asilimia 16.4 wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.

Vituo vingi vya kupigia kura vimewekwa shuleni na katika vituo vya kutoa huduma za kijamii.

Matokeo ya baadhi ya majimbo yanatarajiwa kutangazwa leo  usiku huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa Ijumaa mchana.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment