Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, May 2, 2014

Mkapa atoa hadhari kuhusu Katiba Mpya


Rais mstaafu, Benjamin Mkapa akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone kwenye viwanja vya zahanati ya Kijiji cha Senenemfuru, wilaya ya Singida kuzindua nyumba za watumishi zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa. Picha na Gasper Andrew 
Na Gasper Andrew, mwananchi
Singida. Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amewataka Watanzania kuwa waangalifu ili mchakato wa Katiba Mpya usiwe sababu ya kupigana au kufarakana ili kupata Katiba itakayoendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na ushirikiano.
Mkapa alitoa wito huo juzi, alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi nyumba 30 za watumishi wa vituo vya huduma ya afya mkoani hapa zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa HIV/AIDS Foundation kwa zaidi ya Sh1.9 bilioni.
“Vyovyote mchakato wa Katiba utakavyoishia, tuhakikishe tunabaki na amani na utulivu wetu kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu, tuhitilafiane bila kupigana,” alisema.
Alisema Watanzania wanapaswa kwa pamoja wasiiharibu nchi yao na kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho, vinaendelea kuwaenzi waasisi wa Taifa kwa uadilifu mkubwa.
Akabidhi nyumba
Akikabidhi nyumba hizo, Mkapa alisema ana imani wananchi wanaohudumiwa na zahanati 15 zilizojengewa nyumba hizo wataendelea kufaidika na huduma bora kwa kuwa watumishi wameboreshewa mazingira ya kazi.
“Kama mnavyoona nyumba hizi ni za kisasa, zina maeneo muhimu yote yanayokidhi mahitaji ya binadamu, zipo imara na zimekidhi viwango vya ujenzi vinavyostahili,” alisema.
Aliitaka halmashauri zinazohusika kuhakikisha nyumba hizo zinatumika kama ilivyokusudiwa, kutunzwa vizuri na kutengewa bajeti ya kutosha kwa ajili ya ukarabati pale utakapohitajika ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Vijiji vilivyonufaika vipo katika wilaya za Singida Vijijini, Iramba na Manyoni.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment