Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, February 23, 2014

Ukraine yapata rais wa muda

Rais wa muda wa Ukraine Oleksander Turchinov
Bunge la Ukraine limemteua spika kuwa rais wa muda, siku moja baada ya kupiga kura kumtoa madarakani Rais Viktor Yanukovich kufuatia maandamano makubwa.
Spika, Oleksander Turchinov, aliwasihi wabunge wakubaliane juu ya serikali ya umoja wa taifa ifikapo Jumaane.
Chama cha Yanukovych kinasema wa kulaumiwa kwa ghasia zilizotokea Kiev na kuuwa zaidi ya watu 80, ni Bwana Yanukovych mwenyewe na watu walio karibu naye.Yeye ni mshirika mkubwa wa waziri mkuu wa zamani, Yulia Tymoshenko, ambaye alifunguliwa kutoka gerezani Jumamosi.
Rais huyo aliyeng'olewa amekimbia kutoka mji mkuu na amri imetolewa kuwa maafisa wakuu wa zamani wakamatwe kwa mauaji hayo.
Maelfu ya watu bado wako katika medani ya Uhuru, chimbuko la maandamano.
Chanzo: bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment