Writen by
sadataley
6:19 PM
-
0
Comments
Vikosi vya usalama nchini Tunisia vimeizingira nyumba moja iliopo katika kitongoji kimoja cha mji mkuu Tunis,ambapo afisa mmoja wa polisi na washukiwa wawili wanaotuhumiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu waliuawa wakati wa makabiliano ya risasi hapo jana jumatatu.

Tunisia yakabiliwa na mzozo wa kigaidi.
Maafisa wanasema ufyatulianaji wa risasi ulianza wakati maafisa wa polisi walipojaribu kuvamia nyumba hiyo kufuatia habari kwamba wapiganaji waliokuwa wamejihami na silaha kali walikuwa ndani.
Polisi hao kwa sasa wanajadiliana na wapiganaji hao wakiwataka wajisalimishe.
Tishio la itikadi kali za kiislamu,limeongezeka nchini Tunisia kufuatia shambulizi la ulipuaji wa kujitolea muhanga baada ya kipindi cha miaka kumi katika hoteli moja mwaka uliopita.
Mauaji ya viongozi wawili wa upinzani pia yanadaiwa kutekelezwa na wanamgambo hao wa kiislamu.
No comments
Post a Comment