Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, February 22, 2014

Marekani yaunga mkataba wa Ukrain

Ikulu ya whitehouse nchini Marekani imefurahishwa na makubaliano yalioafikiwa kati ya rais Victor Yanukovych na Upinzani katika hatua ya kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Ukrain.

viongozi wa Ukrain na Urusi watia sahihi mkataba
Afisa mmoja wa marekani Jay Carney amesema kuwa rais Obama alizungumza na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin ambaye amesema kuwa Urusi inataka kushirikishwa katika utekelezaji wa mkataba huo.
Aidha makubaliano hayo yanarejesha sheria ya kumpunguzia mamlaka rais,swala ambalo tayari limepitishwa na bunge.Kulingana na mkataba huo uliosimamiwa na mawaziri wa maswala ya kigeni kutoka umoja wa bara ulaya,serikali ya mpito itabuniwa na Uchaguzi kufanywa mwezi wa Disemba.
Aidha bunge lilipitisha sheria ambayo itamuachilia huru kongozi wa Upinzani Yulia Tymoshenko.
Wakati huohuo makumi ya maelfu ya waandamanaji bado wamesalia katika medani ya uhuru katikati ya mji mkuu wa Kiev usiku kucha.
Waandishi wanasema kuwa waandamanaji hao wana hofu kwamba huenda mkataba huo usitekelezwe.
Waandamanaji hao waliwazoma viongozi wa upinzani waliposimama katika jukwaa ili kuwahutubia baada ya kutia sahihi mkataba huo.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kundi moja la waandamanaji limetishia kuvamia majengo ya bunge iwapo rais Yanukovych hatajiuzulu kufikia leo asubuhi.
Awali kulikuwa na matukio ya kusikitisha baada ya majeneza ya watu 77 waliouawa wakati wa siku tatu za ghasia hizo kuwasilishwa katika medani ya uhuru.
Chanzo:bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment