Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, February 23, 2014

Bunge la Ukraine lamtimua Yanukovych

Waandamanaji Ukraine
Mambo yanabadilika haraka mjini Kiev, mji mkuu wa Ukraine, baada ya maafikiano ya Ijumaa kumaliza msukosuko mkubwa wa nchi hiyo.
Bunge la Ukraine limepiga kura kumshtaki Rais Yanukovych.
Baada ya hatua hizo kupitishwa wabunge walipiga makofi na kuimba wimbo wa taifa.Na wabunge piya wametaja siku ya uchaguzi mpya kuwa tarehe 25 May.
Na hapo awali bunge limepiga kura kumtoa gerezani kiongozi wa upinzani, Yulia Tymoshenko, baada ya washirika wake wawili kuteuliwa kuwa spika wa bunge na waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Spika mpya, Alexander Turchinov, ndiye atayeratibu shughuli za serikali hadi utawala mpya utapoundwa.
Huku nyuma, msaidizi wa Rais Yanukovych amesema rais sasa yuko mji wa Kharkiv, mashariki mwa nchi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment