Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, December 30, 2013

Mchakato wa Wajumbe wa Bunge la Katiba waanza

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utaratibu wa kupata majina ya wajumbe watakaoteuliwa kwenye  Bunge la Katiba. Picha na Fidelis Felix. 
Na Aidan Mhando, Mwananchi
Dar es Salaam. Vyama vya siasa, wafanyakazi, walemavu na makundi mengine ya watu maalumu, leo wanaanza mchakato wa uteuzi wa majina ya watu wanaotaka kuomba nafasi ya kuchaguliwa kuingia kwenye Bunge la Katiba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe aliyoitoa mwishoni mwa wiki, ilisema mpaka kufikia Januari 2 mwakani,  majina ya watu hao yanatakiwa kuwa yamefika mahali husika ili uteuzi uanze kufanyika.
Kwa mujibu wa Chikawe, makundi hayo yanajumuisha  wajumbe 20 kutoka  taasisi zisizokuwa za kiserikali na nusu yao lazima wawe wanawake na moja ya tatu watatoka Zanzibar.
Pia wajumbe 20 watatoka taasisi zote za dini, wajumbe 42 kutoka vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu.
Kwa mujibu wa mchanganua huo, kati ya vyama 21 kila chama kitatoa  wajumbe wawili na kwamba kwa vyama vya siasa ni lazima mjumbe mmoja atoke Zanzibar na mmoja awe mwanamke na mwingine mwanamume.
Wajumbe wengine wanatoka taasisi za Elimu ya Juu watakuwa (20), makundi ya watu wenye ulemavu (20), vyama vya wafanyakazi (19), vyama vinavyowawakilisha wafugaji (10), vyama vinavyowawakilisha wavuvi (10) na vyama vya wakulima (20). Katika nafasi hizo, pia zimetengwa 20 kwa ajili ya wajumbe kutoka makundi mengine yenye malengo yanayofanana.
Pia wajumbe 20 watatoka kwenye taasisi zisizokuwa za kiserikali na nusu yao lazima wawe wanawake.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment