Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, December 27, 2013

BAADHI YA PICHA ZA TAMASHA LA KRISMASI UWANJA WA TAIFA DAR

Kwa ambaye hakufika jana katika tamasha la Krismasi ambalo limeandaliwa na kampuni ya kimataifa ya kuandaa matamasha ya Msama Promotions ambapo waimbaji kadhaa kutoka ndani na nje ya nchi walikuwepo.

Funika ya wote alikuwa Mchungaji Solly Mahlangu, (tutakuwekea video kadri zitakavyokuwa tayari) na perfomance yake haikuchosha, na hata anaondoka akawatia moyo waimbaji na kuwashauri kuhudumu chini ya wachungaji wao kwa uaminifu, na sio kurukaruka tu hapa na pale. Na kubwa zaidi kwa wote, akasema Love Life, AIDS Kills, yaani Yapende Maisha, UKIMWI Unaua.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika tamasha hilo, Waziri wa Nchi - Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mheshimiwa William Lukuvi alionekana kuguswa na jambo la Msama Promotions kufikia hatua ya kuwezesha matamasha mawili ya kimataifa kwa mwaka, yaani lile la Pasaka na la hili la Krismasi.

Tamasha hilo ambalo lilikuwa na changamoto za hapa na pale ikiwemo la umeme kusumbua mfumo wa ufanisi kazi wa mixer, lilibadilika mwelekeo kutokana na live perfomance ya Son of Tanzania Ephraim Sekeleti akishirikiana na Living Water, na kisha aliyefunga kazi akawa Solly Mahlangu.  Endelea kutembelea GK kwa ajili ya picha na video zaidi za tamasha hilo.

Kwa leo, msafara wa waimbaji uko Morogoro, kabla ya kuelekea Tanga na kisha Arusha.

Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi - Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, Mh. William Lukuvi


Paul Clement na GWT wakimsindikiza Ephraim Sekeleti.

John Lisu na gitaa lake
Upendo Nkone akiwa jukwaani.



Living Water wakiwa kazini

Unaweeeeeeeezaaaaaaa, drum zikiisindikiza.



Mh Ezekiel Maige, aliyemsindikiza mgeni rasmi, William Lukuvi


John Lisu akiwa na back up wake

Waimbaji mbalimbali wakishambulia jukwaa kwa pamoja na Solly Mahlangu

Solly Mahlangu

New Life Band kutoka Arusha.

Habari kwa hisani ya Gopsel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment