Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, December 15, 2013

ANC watoa heshima kwa mwili wa Mandela

Wanachama wa Chama cha African National Congress (ANC) wametoa heshima za mwisho kwenye mwili wa Hayati Nelson Mandela kabla ya kuzikwa hapo kesho.
Rais Jacob Zuma na viongozi wengine wa ANC walihudhuria tukio hilo iliyopambwa na sala za viongozi wa mbali mbali wa dini pamoja na muziki.
Karibu watu wanachama 1000 wa ANC ambacho kiliwahi kuongozwa na Hayati Mandela wamehudhuria zoezi hilo la kutoa heshima za mwisho kwenye ngome ya jeshi la anga Waterkloof mjini Pretoria. Hata hivyo si wote waliopata nafasi ya kutoa heshima.
Mwanaharakati anayepigania haki za watu weusi nchini Marekani Jesse Jackson na kiongozi wa Ireland Sinn Fein Gerry Adams ni miongoni mwa viongozi wa kimataifa waliohudhuria hafla hiyo
Baadae jeneza la Mandela litachukuliwa kwa ndege kwenda katika kijiji cha Qunu katika jimbo la Cape ya Mashariki.
Jeneza hilo litasindikizwa na wanafamilia na maafisa wa serikali.
Hayati Mandela alifariki Decemba 5, mwaka huu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment