Writen by
sadataley
8:53 AM
-
0
Comments
Ni mkoani Tabora, ambapo waumini wa Kiislamu watajumuika pamoja kitaifa kusherehekea sikukuu hiyo.
Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal
Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal anatarajiwa kuongoza Swala ya Eid el Fitr itakayoswaliwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa alisema jana kuwa baada ya swala hiyo, itafuatiwa na Baraza la Eid itakayofanyika mkoani Tabora na kushirikisha viongozi mbalimbali wa nchi.
“Naomba nichukue nafasi hii kulishukuru Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Bakwata kwa kuifanya Sikukuu ya Eid el Fitr kitaifa mkoani kwetu,” alisema.
Mwassa alisema baada ya swala hiyo, Makamu wa Rais atakayefuatana na mkewe watakula chakula cha pamoja na watoto yatima wa mjini Tabora.
Wakati huohuo, Waislamu wa madhehebu ya Answar Sunn jana waliswali swala ya Eid el Fitr katika maeneo mbalimbali nchini.
Gazeti hili lilishuhudia swala hiyo katika maeneo ya Jangwani, Mnazi Mmoja, Mabibo External na maeneo mengine.
Akihutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam, Sheikh Issa Mohamed kutoka Iringa, aliwataka Waislamu kuepuka makundi ndani ya dini hiyo na badala yake wafuate maagizo na sheria alizoziacha Mtume Mohamed (SAW).
“Kuna makundi ya upotoshaji ambayo hayataki kufuata sheria za Mwenyezi Mungu, hawataki kukubaliana na siku zote wao wanatumiwa na makundi hayo kuivuruga hata siku ya mwezi kuandamana,”alisema Sheikh Issa.
Wakati huohuo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametoa zawadi ya Eid el Fitr yenye dhamani ya Sh8,490,000 kwa makundi maalumu, wakiwamo watoto wenye ulemavu,wazee,yatima pamoja na watoto walio katika mkinzano na sharia ili kuwaandalia mazingira mazuri ya kuwezesha kushiriki na kusherehekea sikukuu hiyo.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Rabikira Mushi alikabidhi vifaa hivyo jana kwa niaba ya rais katika hafla iliyofanyika katika Mahabusu ya Watoto Kisutu na kuhudhuriwa na wawakilishi wa vituo husika alisema, Rais ametoa zawadi ya mchele, mafuta ya kupikia pamoja na mbuzi kwa baadhi ya vituo nchini kwa lengo la kufurahia siku hiyo.
Habari kutoka Gazeti la mwananchi
No comments
Post a Comment