Writen by
sadataley
3:31 PM
-
0
Comments
Leo March 27, 2018 Viongozi Wakuu wa CHADEMA akiwepo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene imeeleza kuwa Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo ila Mawakili wanashughulikia.
“Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na Wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya DSM wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi,” -Makene
“Viongozi wa CHADEMA wanaoshikiliwa Polisi ni Mwenyekiti wa CDM Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dr. Vincent Mashinji, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalim, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na Ester Matiko Mbunge” -Tumain Makene
Millardayo
No comments
Post a Comment