Writen by
sadataley
11:31 AM
-
0
Comments
Mbunge wa zamani wa Kongresi ya Marekani amesema Rais Donald Trump wa nchi hiyo amekiuka ahadi aliyotoa wakati wa kampeni za urais kwamba akiingia madarakani hataitumbukzia tena nchi hiyo katika vita.
Ron Paul ambaye alichuana bila mafanikio katika kura ya mchujo ya chama wa Republican kwa ajili ya kugombea urais nchini Marekani mwaka 2008 na 2012, amesema, iwapo Trump ataiingiza nchi hiyo katika vita ama na Iran au Korea Kaskazini, basi huo ndio utakuwa mwisho wa utawala wake.
Paul mwenye umri wa miaka 81 amechapisha makala katika tovuti ya taasisi yake inayoitwa Ron Paul Institute for Peace and Prosperity akisisitiza kuwa, licha ya Tehran kutekeleza kikamilifu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, lakini serikali ya Trump imekuwa ikiendeleza chokochoko dhidi ya taifa hilo na kutafuta vijisababu vya kuanzisha vita dhidi ya Iran.
Mwanasiasa huyo mkongwe wa Marekani amesema kitendo cha hivi karibuni cha jeshi la Marekani cha kurusha katika anga ya Peninsula ya Korea ndege yake ya kivita ya US B-1 yenye uwezo mkubwa wa kudondosha mabomu ni ithibati tosha kuwa Trump yuko tayari kuishambulia Pyongyanga pasina na kuzingatia taathira zake hasi.
Katika kutamatisha makala hiyo, Ron Paul amenukuu uchunguzi uliofanywa na vyuo vikuu vya Boston na Minnesota uliobainisha kuwa, Trump alizoa kura nyingi katika majimbo ya Wisconsin, Pennsylvania na Michigan, yenye idadi kubwa ya familia za wahanga wa hatua za kijeshi za Marekani, wakitaraji kuwa mwanasiasa huyo hataiingiza tena nchi hiyo katika vita na uvamizi dhidi ya nchi nyingine.
Parstoday
No comments
Post a Comment