Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 29, 2017

JPM aipa Tano TCU kuvifunga vyuo 19


WAKATI wamiliki wa vyuo 19 wakiendelea kusikilizia maumivu baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuviamuru kusitisha udahili wa wanafunzi kwa mwaka huu wa masomo, Rais John Magufuli ameweka msimamo kuhusu tamko la tume hiyo.


Wiki hii, TCU ilivizuia vyuo 19 kudahili wanafunzi na kuvizuia vingine kudahili wanafunzi kwenye kozi 75  katika vyuo 22 ambazo ilisema haizitambui.

Akizungumza na wakazi wa Tegeta, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati akitokea mikoani alikokuwa katika ziara ya kikazi, Rais Magufuli aliipongeza hatua ambayo TCU imechukua.

“Ndugu zangu nchi hii ilishakuwa kila kitu hewa, tumegundua wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, kulikuwa na mikopo hewa ya wanafunzi. Ninapongeza TCU kwa kufungia baadhi ya vyuo kudahili wanafunzi. Nafanya yote haya kwa ajili yenu, nataka tuwe na nchi nzuri” alisema Magufuli.

Rais Magufuli alisema kwa kuwa ni mara yake ya kwanza kupita Tegeta, amelazimika kusimamisha msafara wake kuwashukuru wananchi kwa kumweka Mungu mbele na kumchagua mtu ambaye atalisaidia taifa.

“Kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kusimama hapa Tegeta, nianze kwa kuwashukuru sana kwa kura nyingi mlizonipa ili niwe Rais wa Awamu ya Tano. Nawashukuru CCM, nawashukuru Chadema, nawashukuru CUF, nawashukuru ACT na hata wale ambao hawana chama kwani wote kwa umoja wenu mlitanguliza maslahi ya taifa na kumpa kura mtu ambaye atalisaidia taifa.

“Na mimi nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote na kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu ili kuwaletea maendeleo Watanzania wote hasa wanyonge ambao siku zote walikuwa wakionewa,” alisema Magufuli.

Jumatatu ya wiki hii, Kaimu  Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Eleuther Mwageni, katika taarifa yake, alieleza kuwa Tume ilifanya uhakiki kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu Septemba na Oktoba, mwaka jana, ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni.

Aidha, alisema ripoti ya uhakiki ilionyesha upungufu kadhaa katika baadhi ya vyuo, hivyo kuamua kusitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo 19.

Alivitaja vyuo hivyo na mkoa kilipo kwenye mabado kuwa ni Eckenford (Tanga), Jomo Kenyatta (Arusha), United African University of Tanzania, International Medical and Technological (IMTU) na Bagamoyo.

Vingine ni St. Francis, Archibishop Mihayo, Kampala International, Marian, St. Johns, St.  Joseph, Teofilo Kisanji, Tumaini Mbeya na KCMC

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment