Monday, December 16, 2013

Kocha wa Tottehnam atimuliwa baada ya timu yake kutibuliwa kwa mabao 5 kwa nunge

Are Villas-Boas, kocha wa Tottehnam alietimuliwa
Are Villas-Boas, kocha wa Tottehnam alietimuliwa
© Reuters

Na RFI
Tottehnam imejitenga na kocha wake, Andre Villas-Boas ambae ni raia wa Ureno. Boas alijiunga na timu hio toka mwaka 2012. Tottehnam imejitenga na Andre Villas-Boas, baada ya kushindwa kufanya vizuri nyumbani kwa kunyeshewa mvua ya mabao (5-0) na Liverpool, wakati ilikua ni miaka 16 timu hio haijafungwa na Liverpool.

Klabu hio imefahamisha kwamba uamzi huo umechukuliwa pande zote mbili (Tottenham na Andre Villas-Boas) zikiafikiana.
Villas-Boas, mwenye umri wa miaka 36 alifutwa kazi na timu yake ya mwanzo, chelsea, ilikua mwezi machi mwaka 2012, baada ya miezi 9 akiipa mafunzo timu hio.
Villas-Boas, alijiandikishia jina wakati FC Porto iliibuka mshindi katika michuano ya Kombe la Ureno na michuano ya Kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Na hatimaye, timu ambazo zitakutana katika mzunguuko wa nane katika michuanao ya klabu bingwa barani Ulaya, zimejulikana leo. Manchester City itaminyana na FC Barcelona, huku Bayern Munich ikikutana na Arsenal.
Mzunguuko wa kwanza utachezwa tarehe 18-19 mwezi februari ao tarehe 25-26 mwezi februari, na mechi za marudiano zichezwe tarehe 11-12 mwezi machi ao tarehe 18-19 mwezi machi
Man City imeibuka mshindi jana jumapili kwa kuifunga Arsenal mabao (6-3).

No comments:

Post a Comment