Thursday, August 1, 2013

MATOKEO YA MUDA YA UCHAGUZI WA MALI KUTOLEWA ALHAMISI

Maafisa huko Mali wanatarajiwa kutoa matokeo ya muda ya uchaguzi wa rais nchini humo alhamisi.
Muunga mkono wa mgombea Ibrahim Boubacar Keita akishikilia bendera kabla ya chama chake.
 Muunga mkono wa mgombea Ibrahim Boubacar Keita akishikilia bendera kabla ya chama chake.

Upigaji kura wa jumapili ulionekana kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye  kurejesha Mali katika hali ya kawaida baada ya machafuko ya mwaka mmoja na nusu.

Jumanne waziri wa tawala za kieneo Kanali Moussa Sinko Coulibaly matokeo ya mwanzo yanaonyesha mgombea anayeongoza ni waziri mkuu wa zamani  Ibrahim Boubacar Keita  alikuwa akiongoza kwa kiasi kikubwa na anaweza kushinda bila taabu.
Hakueleza  tofauti hiyo ya ukubwa lakini alisema kama ikibaki hivyo hakutakuwa na uchaguzi wa marudio.

Imewekwa na Happy Adam

No comments:

Post a Comment