Wednesday, August 2, 2017

Waziri Lukuvi awatahadharisha wananchi juu ya matapeli wa nyaraka za umiliki ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amekutana na wakazi wa Wilaya ya Temeke na Kigamboni katika kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi. Katika mahojiano na wananchi hao, Mhe. Lukuvi amewaonya wananchi kuwa makini na matapeli wanaochukua nyaraka halali za umiliki na kutengeza nyaraka feki.

Hayo yamebainika baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia mmliki wa kampuni ya Holland Investment iliyopo  jijini Dar es Salaam kwamba, amekuwa akichukua nyaraka halali za umiliki kwa wananchi kwa lengo la kuwasaidia na baadae kuwabadilishia na kuwarudishia nyaraka feki.

No comments:

Post a Comment