Thursday, August 3, 2017

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi aidhinisha kura za wananchi na kumpasisha Rouhani kuwa Rais wa Iran

Sherehe ya kuidhinisha kura za wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu zimefanyika leo asubuhi katika Husseiniya ya Imamu Khomeini (M.A) hapa Tehran kwa Kiongozi Muamdhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumpasisha Hassan Rouhani kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi akimpongeza Rais Rouhani katika hafla hiyo.
Kitengo cha Habari cha Kiongozi Muadhamu kimeripoti kuwa, Ayatullah Khamenei katika dikrii aliyotoa katika sherehe hiyo ameutaja uchaguzi uliohudhuriwa na wananchi wengi na kupata kura nyingi shakhsiya aliyechaguliwa kuwa ni ishara ya kuimarika Mfumo wa Jamhuri na amesisitiza udharura wa kutekelezwa mpango wa uchumi wa ngangari. 
Ayatullah Khamenei amemtaka Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuelekeza jitihada zake katika kutekeleza uadilifu, kuwatetea wale wote walionyongeshwa na maskini, kutekeleza sheria za Kiislamu, kuimarisha umoja na heshima ya taifa na kutilia maanani uwezo mkubwa wa nchi na kuwa wazi katika kutukuza thamani na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu.  
katika sherehe hiyo pia Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran ametoa ripoti kuhusu namna uchaguzi wa 12 wa Rais ulivyofanyika hapa nchini.
Kwa mujibu wa kifungu cha 110 cha Katiba ya Iran, miongoni mwa majukumu na mamlaka ya Kiongozi Muadhamu ni kusaini na kupasisha dikrii ya Rais wa nchi baada ya kuchaguliwa na wananchi. Kipindi cha urais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miaka minne na Rais huanza kutumikia wadhifa wake baada ya tarehe ya kuidhinishwa hati za utambulisho wake na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Hassan Rouhani kwa mara nyingine tena alichaguliwa kuwa Rais wa Iran katika duru ya 12 ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika Mei 19 mwaka huu kwa kupata kura zaidi ya milioni 23.

Parstoday

No comments:

Post a Comment