Sunday, July 30, 2017

Tanzania yashika nafasi ya pili barani Afrika kwa uzalishaji wa zao la alizeti.

Tanzania imetanjwa kuwa ni nchi ya pili barani Afrika kwa uzalishaji wa zao la alizeti baada ya Afrika Kusini.

Kauli hiyo imetolewa katika uzinduzi wa kuimarisha mfumo wa soko la alizeti katika nmikoa ya Mtwara na Lindi ambapo meneja wa mradi huo MARTINI MGALLAH amesema fursa ya kibiashara kwa zao la alizeti nchini bado ni kubwa, hivyo serikali ina kila sababu ya kuwekeza kwenye zao hilo.

Amesema mradi huo umezinduliwa katika mikoa kumi na miwili kwa lengo la kuwahamasisha wakulima wa zao hilo ambalo mafuta yake yanasoko kubwa katika mataifa mbalimbali.

Hata hivyo, pamoja na  baadhi ya wakulima wanaolima zao hilo kusema limekuwa likifanya vizuri, tatizo kubwa ni masoko na ushindani wa mafuta kutoka nje ya nchi ukiwa ni mkubwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo  Naliendele Dakta OMAR MPONDA amesema mpaka taasisi hiyo imegundua na kuzifanyia utafiti aina tatu za mbegu za alizeti ambazo zitapelekwa kwa wakulima kwa ajili ya majaribio.

No comments:

Post a Comment