MIAKA 30 YA NDOA YA MWALIMU CHRISTOPHER NA DIANA MWAKASEGE
Hatimaye Mwalimu Christopher na Diana Mwakasege wamefikisha miaka 30 ya ndoa yao. Ambapo kulikuwa na tafrija fupi ya kusherehekea tendo hilo iliyofanyika jijini Arusha wiki iliyopita ambayo ilihudhuriwa na mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini Askofu dkt Alex Gehaz Malasusa, familia ya mwalimu Mwakasege, ndugu, jamaa pamoja na marafiki. Mungu aendelee kuwainua watumishi hawa ambao wamekuwa baraka kwa taifa letu la Tanzania. Tunawapongeza sana na kuwatakia maisha marefu zaidi ya ndoa pamoja na baraka zitokazo kwa Mungu ziambatane pamoja nanyi siku zote mkazidi kupata maarifa zaidi katika kuwahudumia watu wake.
Picha za tukio ambazo GK imefanikiwa kuzipata.
Mwalimu Mwakasege, mkewe pamoja na mtoto wao wa kiume.
No comments:
Post a Comment