Tuesday, August 28, 2018

HAWA GHASIA AJIUZULU UENYEKITI KAMAYI YA BUNGE YA BAJETI

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Soni wamejiuzulu nafasi hizo. Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai amethibitisha taarifa hizi.

Ghasia ambaye ni mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) na Soni (Babati Vijijini), wametangaza uamuzi wao huo leo asubuhi mjini Dodoma mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.

Bado haijafahamika sababu za viongozi hao kufanya uamuzi ho wa kujiuzulu. 
CCM Blog

No comments:

Post a Comment