Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ameongoza mazishi ya mwanaharakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela ambaye amezikwa leo Jumamosi nchini humo.
Madikizela-Mandela, shujaa wa mapambano ya kudai uhuru wa Afrika Kusini na mke wa zamani wa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela, alifariki dunia Aprili 2 akiwa na umri wa miaka 81.
mezikwa kwa heshima za kitaifa, ambapo maelfu ya waombolezaji wamekusanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Soweto ulio karibu na makazi ya Winnie Madikizela-Mandela.
Marais wa zamani Jacob Zuma na Thabo Mbeki pia nao wamehudhuria mazishi hayo.




No comments:
Post a Comment