Friday, April 6, 2018

Wambura ashindwa rufaa yake, adhabu yake itaendelea


Kamati Ya Rufaa Maadili Ya TFF baada ya kupitia rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo,Michael Richard Wambura imetupilia madai yake yote na adhabu yake itaendelea kama ilivyoamuliwa na  Kamati ya Maadili ya TFF kwa kufungia kutojihusisha na soka maisha yake yote.

Mbali na hilo pia kamati hiyo ya rufaa imeshauri, Wambura afikishwe kwenye vyombo vya dola ili suala hilo liweze kushughulikiwa zaidi na wataalam.

No comments:

Post a Comment