Thursday, April 5, 2018

Twiga Stars yatoka sare na Zambia ‘Shepolopolo’ Taifa

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars imelazimishwa sare ya mabao 3 – 3 uwanja wa Taifa dhidi ya Zambia (Shepolopolo) kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake AFCON 2018 nchini Ghana.

Stars italazimika kuchomoza na ushindi wa aina yoyote wakiwa ugenini nchini Zambia kama wanahitaji kuendelea na mashindano hayo.

Mshindi wa jumla kwa raundi hii atacheza na mshindi kati ya Namibia v Zimbabwe mwezi Mei, na atakayeibuka mshindi atafuzu moja kwa moja kwa Fainali hizo za Wanawake Afrika.

No comments:

Post a Comment