Thursday, April 12, 2018

Serikali ya Algeria yatangaza siku tatu za maombolezo

Serikali ya Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo kwa taifa hilo baada ya jana kutokea ajali ya ndege ya kijechi iliyoua watu 300 muda mfupi tu baada ya kupaa.

Ndege, ambayo inadaiwa kuwa ilikuwa imebeba askari na familia zao, ilianguka muda mfupi tu baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik

Serikali ya Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo kitaifa kufuatia mkasa huo mbaya ambapo tiyari pia vingozi kadhaa akiwemo Mkuu wa Majehi ya Aljeria Generali Ahmed Gaid Salaha amezuru eneo la ajali.

Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika ameagiza kuswaliwa siku ya Ijumaa Sala maalumu kwa maremu baada ya sala tukufu ya Ijumaa.

Ndege hiyo ilianguka katika katika shamba muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik huko Blida, kusini mwa Algiers.

No comments:

Post a Comment