Monday, April 16, 2018

Okwi afikia magoli ya Tambwe, Bocco

Mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba, leo amefunga bao lake la 19 katika Ligi Kuu Bara.

Okwi amefunga bao moja wakati Simba ikiitwanga Prisons kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao la 19, linamfanya Okwi kufikia rekodi mbili za wafungaji Amissi Tambwe na John Bocco ambaye kwa sasa ni nahodha wake.

Bocco aliwahi kufunga mabao 19 na kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara na Tambwe akafanya hivyo na kuwa mfungaji bora.

Kwa kuwa Simba bado ina mechi nyingine sita, maana yake Okwi ana nafasi ya kufikisha mabao 20 au zaidi kama ataendelea kufunga tena.

No comments:

Post a Comment