Saturday, December 21, 2013

Marekani kutuma mjumbe Sudan Kusini

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema atatuma mjumbe maalum nchini Sudan Kusini Bwana Donald Booth kwenda katika mji mkuu wa Juba kusaidia kushawishi mazungumzo ya pande mbili zinazopingana.
John Kerry Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
Kwa wiki nzima sasa mapigano ya kikabila yamesababisha mauaji ya watu karibu 500 nchini Sudan Kusini.
Bwana Kerry ametaka viongozi wa kisiasa wa Sudan Kusini kuwadhibiti wapiganaji wenye silaha.
Afisa wa ngazi za juu wa Ufaransa ambaye ni balozi wa Ufaransa ndani ya Umoja wa Mataifa Gerard Araud amesema mpinzani wa Rais Salva Kiir , Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Riek Machar tangu siku ya Alhamisi wakati alipohojiwa na Radio ya Ufaransa alisema anajianda kuzungumzia kuhusu kujiuzulu kwa rais.
Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi jirani na Sudan Kusini wanatarajiwa kufanya juhudi za kuwezesha mazungumzo ya amani baadae leo.

No comments:

Post a Comment