Saturday, December 21, 2013

JE UNALIJUA HILI KUHUSU PAPA FRANCIS WA KATOLIKI?

Papa Francis akionyesha nembo ya timu ya San Lorenzo anayoshabikia.©thegurdian

Hii leo ipo kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ambaye ni Papa wa kwanza katika historia ya viongozi wa kanisa hilo kutokea Amerika ya kusini. Hivi karibuni katika habari ndani ya GK tulikuandikia namna kiongozi huyu alivyokuwa akiwajibika toka alipokuwa seminari huko nchini Argentina ambako alishiriki katika kufua na kufanya usafi katika seminari aliyokuwa akisomea lakini pia aliwahi kuwa baunsa katika klabu za usiku kabla hajajiunga masomo ya upadri.

Papa huyu ambaye ametimiza miaka 77 juzi na kufanya tafrija ndani ya Vatican imeelezwa kwamba ni mpenzi sana wa mpira wa miguu akiwa anashabikia timu ya San Lorenzo ambayo imetwaa ubingwa wa Argentina hivi karibuni. Katika kuonyesha ushabiki wake katika siku hiyo ya kusheherekea birthday yake alitembelewa na ujumbe wa timu hiyo ambayo licha ya kuwa na mazungumzo naye walimpa zawadi ya fulana ya timu hiyo.

Papa Francis akiwa na viongozi wa timu ya San Lorenzo siku ya jumanne wiki hii walipomtembelea na kumkabidhi jezi yenye jina lake.
Papa Francis anazungumzwa kama mmoja wa viongozi wa kanisa Katoliki walioanza vyema uongozi wao kwakutaka kanisa kusimama katika zamu zao kwakusaidia watu wasiojiweza na wenye uhitaji, kuliko kukaa tu makanisani na kuzungumza habari za Yesu wakati watu wengine wanateseka.KWA TAARIFA YAKO kama hujui Papa huyo pia tangu kuingia kwake madarakani hajawahi kuzungumzia suala la mapenzi ya jinsia moja katika mahubiri yake huku watu mbalimbali wakisubiri kwa hamu kusikia msimamo wake kuhusu masuala hayo.

Papa Francis akiwa na mchezaji matata Mario Baloteli mjini Vatican mapema mwezi August mwaka huu. ©The Guardian.
Gazeti linaloongoza kwakupigania haki za mapenzi ya jinsia moja liitwalo "The Advocates magazine" limemtangaza Papa Francis kama mtu wa mfano kwa mwaka 2013. 

No comments:

Post a Comment