
Afisa huyo amesema meli yeyote itakayotia nanga katika bandari za Libya bila idhini ya serikali itashambuliwa kwa bomu.Wafanyikazi wa badari wamekua kwenye mgomo wiki kadhaa sasa kulalamikia malipo. Maafisa wamesema mgomo huo umesababisha kupungua kwa mauzo ya mafuta nchini Libya na hivyo kuathiri vibaya uchumi wa nchi.
Waziri Mkuu amesema serikali itatumia nguvu zozote zile kuzuia kile amesema kuvuruga biashara ya mafuta. Banadari zilizoathirika na mgomo ni pamoja na Zeitunia, Brega, Ras Lanouf na Sedra. Uzalishaji wa mafuta Libya ulipungua hadi mapipa laki sita kutoka mapipa milioni moja baada ya kuzuka mapinduzi dhidi ya kiongozi wa zamani Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Imewekwa na Happy Adam
No comments:
Post a Comment