Wednesday, August 14, 2013

KKKT DAYOSISI YA IRINGA YAPATA MSIBA. NI MSIBA WA MKE WA MKUU WA JIMBO LA KASKAZINI MASHARIKI (ILULA) MCHUNGAJI GIDEON MHENGA

Ni mama Mchungaji Gideon Mhenga ambaye alifariki jana huko Dar es salaam, Ibada fupi ya kuuaga mwili wake yafanyika hapa Kanisa la Kilutheri  Ilula na hivi sasa mwili wake upo hapa Iringa Mjini ukisubiri taratibu za  mazishi yatakayofanyika kesho Tarehe 15/8/2013.
Kanisa la Jimboni hapa  Ilula ambapo leo hii ndipo ilipofanyika sala fupi kwaajili ya kuuaga mwili wa mama Mchungaji Gideon Mhenga.
Huo ni mwonekano wa nje wa Kanisa hilo la Jimbo la Ilula pembeni ni baadhi ya waumini wa Kanisa hilo waliohudhurika katika Ibada fupi ya kumuaga Mama Mchungaji Gideon Mhenga.

Ni madhabahu ya Kanisa la Ilula ambapo ndipo palitumika katika kuongoza Ibada iliyofanywa na baadhi ya Wachungaji katika kuuaga mwili wa mama Mchungaji Gideon Mhenga.

Imewekwa na Happy Adam

No comments:

Post a Comment