Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

MATUKIO YA JUBILII YA KKKT

JUBILII YA MIAKA 50 YA
KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
21-24 JUNI, 2013
CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA
Bw.Brighton Kilewa
Katibu Mkuu K.K.K.T
Watu 5000 kuhudhuria maadhimisho ya jubilii Wageni wapatao 5,000 wanatarajiwa kuhudhuria matukio ya kilele cha jubilii ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) tarehe 22 na 23 Juni 2013 kukumbuka miaka 50 tangu Makanisa saba ya Kilutheri nchini kuunganana kuunda Kanisa moja. Katibu Mkuu wa KKKT, Bw. Brighton Killewa alisema hivi karibuni,  kilele kitaadhimishwa katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Tumaini University Makumira -TUMA), Usa River kinachomilikiwa na KKKT kitakuwa na matukio yasiku mbili.

Alisema Juni 22 litakuwepo kongamano ambapo mada tano zitajadiliwa kuhusu kazi za Kanisa miaka 50 iliyopita na nini kifanyike kwa miaka 50 ijayo.
 Siku ya Jumapili 23 Juni ndipo itafanyika Ibada. Tarehe 21 jioni Mkuu wa KKKT anatarajiwa kufungua maonyesho ya kazimbalimbali na usiku kutakuwa na mkesha wa kwaya yenye watu 350.

Kanisa linatarajia wageni wapatao 5,000 toka ndani na nje ya nchi kuhudhuria maadhimisho hayo yatakayofanyika Usa River, nje kidogo ya jiji
 la Arusha. Wageni wa nje ni kutoka makanisa na vyama vya misioni vya  Afrika, Ulaya na Marekani. Kutoka ndani ni pamoja na wawakilishi wa Dayosisi za KKKT, viongozi wa Serikali na wa dini na kwaya.

Chuo cha Makumira ni mojawapo ya vituo vya pamoja kama Kanisa (vijulikanavyo kama vituo vya Kazi za Umoja KKKT) kinachounganisha Dayosisi zote 22 za KKKT. Ni kituo cha mafunzo kilichoanza kama chuo cha Theologia hivyo viongozi wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki, Kati, Kusini na Magharibi mwa Afika na Mashariki ya Mbali (Middle East) wakiwemo Wachungaji na Maaskofu wamesoma katika chuo hicho. Chini ya mpango wakubadilishana wanafunzi baadhi ya wanafunzi na wakufunzi wametoka Ulaya na Marekani.

KKKT ni muungano wa makanisa saba ambayo baadhi yao yalianza kutekeleza utume wa Mungu wa kueneza Injili nchini zaidi ya miaka 150. Tarehe 19 Juni
 1963 viongozi wa Makanisa hayo saba kwa hiari yao waliweka tofauti zao

kando na kuamua kuunda Kanisa moja na kugeuza Makanisa yao kuwa Sinodi au Dayosisi za KKKT. Kadiri muda ulivyokwenda KKKT ikakubaliana kuacha mfumo wa Sinodi na kuwa na mfumo wa Dayosisi.

Hadi 26 Mei 2013 Dayosisi za KKKT zimefikia 22 baada ya mbili kuzinduliwa mwaka huu wa Jubilii. Nazo ni Dayosisi ya Kusini Mashariki (Mtwara/ Lindi) iliyozinduliwa Jumapili 26 Mei 2013 na Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (Shinyanga/ Simiyu) iliyozinduliwa 5 Mei 2013.
Habari  na Elizabeth Lobulu-Afisa Habari K.K.K.T



MADA KUU

1.    THE IMPACT OF GLOBALIZATION ON THE CHURCH IN AFRICA.

2.   THE ROLE OF AFRICAN EVANGELISTS IN THE WESTERN HEMISPHERE.



3.   THE IMPORTANCE OF TEACHING THE FOUNDATION OF FAITH AND PROFESSIONAL ETHICS IN HIGHER LEARNING INSTITUTIONS AND ITS CONTRIBUTION IN BUILDING AN ETHICAL NATION.


4.   NEW AREAS OF MISSION IN 50 YEARS TO COME (NEW STRATEGIES OF FAST GROWING CITIES AND THE ROLE OF EVANGELISM AND DIACONATE, INTEGRITY OF CREATION AND GENDER ISSUES).



5.   FACING THE CHALLENGES OF CHARISMATIC MOVEMENT AND PENTECOSTALISM (Healing and Miracles).




KWA HABARI  NA MATUKIO KATIKA PICHA  YA


 JUBILII HII FUATILIA MTANDAO HUU 

NISAFARI YA KUELEKEA ARUSHA KWENYE JUBILII YA KKKT
                         Mtangazaji wa redio Furaha Noel kaguo tayari kwa safari


Bloger akiwa  Chalinze tayari kwenda Arusha
SASA NI KATIKA JUBILEE YA KKKT  -MAKUMIRA  ARUSHA 
KARIBU  SANA
                            Mtoto Brown Lee toka iringa tayari kushiriki Jubilii hii
hapa ndipo katika Ukumbi ulioboreshwa vizuri kwa ajili ya Jubilii hii

Mchungaji Stephane Homstom Katibu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Sweeden

                                            Askofu na Mchungaji toka Marekani
Wageni toka Ulaya na marekani




    

Baadhi ya wawezeshaji wakwanza Mchg. Dr. Paslaw, Pofesa Bahendwa na Mchg. Dr. Kimondo toka Chuo Kikuu Iringa

Makatibu Wakuu ni Bw. Naymna Chavalla Iringa na   Barozi Maliki toka Mashariki na Pwani
Askofu Mkuu Mstaafu Dr. Mushemba akiwa katika Jubilii hii hivi sasa
HIVI SASA NI KATIKA MADA YA UTANDAWAZI(GLOBALISATION)
INAYOTOLEWA 

PROFESA WINFRED  MLAY
Mkuu KKKT akifuatilia mada kwa umakini mkubwa sana


KWAYA KUU KKKT-DAYOSISI YA IRINGA IKIWA JUKWAANI HIVI SASA
Wimbo "Nimempata rafiki Mwema"
                                                      Kwaya Kuu ikiwa katika Jukwaa

wageni wakisikiliza wimbo kwa umakini

                       Askofu Dr. O.M. Mdegella  akiwa na mama wakifurahi kuiona kwaya toka Iringa



Mchungaji Ester Hauli toka iringa akiwa katika Jubilii hii

                                    Mchungaji Yekonia Koo Katibu wa Vijana Iringa nae alikuwepo
Watheolojia wanaosoma Makumira toka Iringa


                             Mchungaji Mwantepele toka Dayosisi ya Kusini(Njombe)
Maaskofu wastaafu nao wahawakuwa nyuma hapa ni Baba Askofu Mwambungu na Sagaya 

Askofu Gulle toka Mwanza mwenye miwani


                                  Askofu Mjema katikati  akiwa katika Jubilii hii
Askofu Yesaya Mengele  wa pili (Njombe) nae alikuwepo 

                    Katibu wa Berlin Mision -Afrika Mchg. Reinhard Kees akiwa katika Jubilii
                                                            Baadhi ya washiriki

Katibu wa Lutheran World Federation  Ukanda wa Afrika Mchg. Eliesh Mungure 
akitoa itikio la somo la Utandawazo(Globalisation)

WAANDISHI WA RADIO FURAHA  NA UPENDO FM WAKIWA KAZINI TAYARI
Sikiliza Redio Furaha kupitia Blog hii
MATUKIO YA JUBILII KANISA KATIKA PICHA MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA SEHEMU YA KWANZA  KWA ASUBUHI HII
Profesa Festo Bahendwa akiwa na baadhi ya Maaskofu Wastaafu wakitoka nje

Mkuu KKKT  akiwa na Askofu Mstaafu Baba Askofu Kweka

Mwandishi Mwandamizi wa CCT Mchg. Kamoyo akiwa na Mwandishi wa Gazeti la Upengo Miss Manka

Askofu Reinard Mtenji akiwa na Katibu wa Berlin Mision Mchg. Dr. Reinhard Kees


Naibu Katibu Mkuu Mipando na Maendeleo KKKT akiwa na Mchg. Kivambala ambaye ni mmoja wa Wanafunzi toka Dayosisi ya Iringa 

Katibu Mkuu wa Lutheran World Federation akiwa na Katibu Mkuu wa Kanisa la Sweden
PROFESA FESTO BAHENDWA: 
"MATUMIZI YA MTANDAO (INTERNET) YAMESABABISHA KUSHUKA KWA MAADILI NA UTAMADUNI WETU KAMA WAAFRIKA NA WATANZANIA".
1. We have to go back in our normal proper culicullum in our education policy .

2. As far as moral deterioration is a problem in our country what we have to do in life of Tanzania


Mchungaji Profesa Festo Bahendwa 
Hapa akitoa mada ya Changamoto za Mmmomonyoko wa Maadili katika vyuo Vikuu Binafsi na Taifa kwa ujumla leo hii hapa Tumaini University Makumira
MCHUNGAJI DR. STEPHEN KIMONDO "MABADILIKO YA MAADILI YANATEGEMEA MAISHA YA VIONGOZI WA KANISA WANAYOISHI ".


Mchungaji Dr. Stephen Kimondo akitoa itikio la mada ya Maadili katika Vyuo Vikuu Binafsi hapa nchini
KAZI YA UMISIONI HUKO ULAYA 
                                Mbele kabisa ni mnara  unaoelezea wa namna Makumira ilikotoka
Mchg.ALPHAEUS  MLAY akitoa mada

Askofu Dr. Stephen Munga akitoa itikio la mada hiyo
                                          Askofu Dr. Owdenburg Mdegella akichangia katika mada hiyo

                     Baadhi ya Maaskofu Wastaafu wakiwa na baadhi ya Wenzi wa Maaskofu Wastaafu


"HAYA NI WAKATI WA CHAI"  sauti ya  Katibu   Mkuu KKKT ilisikika



                                Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Iringa tayari kwa kifungua kinywa
                                        Mwalimu nguli wa Kwaya Kuu Iringa akipata vitafunwa
                                           Wageni mbalimbali wakijumuika kupata chai
                                         Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa chai
                              Haya na tufurahie chai ni maneno ya baadhi ya wajumbe yalisikika

Wengine wakipata chai, Mabanda ya maonyesho yaliendelea kutembelewa





 Mama Rachel Ramadhani akiwa na Naibu Katibu Mkuu Fedha na Utawala Bw. Abel Mrema
KWAYA ZIKIFANYA   MAZOEZI YA PAMOJA TAYARI KWA IBADA YA  LEO
Zilikuwa zikiongozwa na  Mwl. Randy  Stubbs toka  Marekani 
ambaye ni Mwalimu wa Muziki hapa Chuo Kikuu Tumaini Mkumira



                                          Hapa akipiga kinanda kwa umahiri mkubwa






TAMASHA LA UIMBAJI LILOFANYIKA  KATIKA KANISA LA HAPA CHUONI MAKUMIRA USIKU HUU


Mwl. Obeid Mella  toka Chuo Kikuu Iringa 
ambaye inaaminika kuwa niye mwalimu nguli wa muziki KKKT

Mwl. Habakuki Lwendo toka  Chuo Kikuu Tumaini Makumira




                                   Kwaya toka Dayosisi ya Mashariki na Pwani (Dar)








                                         Nguli wa Muziki Mwl Lwendo akifurahia Uimbaji

                              Mchezaji mahiri wa Ngoma za Asili toka Mashariki na Pwani
                                     Kwaya toka Dayosisi ya Kaskazini kati(Mkoani Arusha)










                               Kwaya toka Dayosisi ya Kaskazini Mashariki(Lushoto-Tanga)






                                                            Baadhi ya Washiriki




                                          Nje ya Kanisa la Makumira (Chapel)

                                  Waimbaji wa Kwaya Kuu Iringa wakifuatilia Uimbaji




                     Kwaya toka Dayosisi ya Kaskazini mwa Ziwa Victoria (Simiyu/Shinyanga)






                                     Kwaya toka Chuo Kikuu Cha Tumaini  Makumira





Kwaya Kuu toka Dayosisi ya  Iringa ikiwa Jukwaani






Mchungaji Dolcus Kimbavalla wa kwanza toka Dayosisi ya Iringa akifurahia Uimbaji
Mmoja wa Wakeleketwa wa Blog hii anayesoma hapa Makumira
WAKATI WA CHAKULA CHA MCHANA  HUWEZI AMINI KUWA NI MAZINGIRA HAYAHAYA YA CHUO CHA MAKUMIRA ANGALIA VIZURI
Mwandishi wa Kanisa akiwa na makatibu Wakuu wa Dayosisi za Iringa na Mashariki na Pwani


Wakuu wa  Majimbo toka Dayosisi ya Iringa Mchg. Donald Kiwanga na Mchg. Himid Sagga 
wakiwa na Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Dodoma 



Wageni wakizungumza wakatika wa chakula

                                            Baadhi ya Wageni toka mataifa mbalimbali




                      Mkuu KKKT akioneshwa picha waliyopiga pamoja na  wageni toka Ulaya
Maaskofu wakijumuika  kupata chakula



                                                    Askofu Gulle akiwa na wageni pia

Askofu Dr. O.M Mdegella toka Dayosisi ya Iringa akiwa na Maaskofu  toka Sweden


                                 Viongozi waandamizi wa Kanisa la Berlin na Lepzing Ujerumani
Askofu Yesaya Mengele akiwa na Katibu Mkuu wa Kanisa la Sweden Mchg Stepahne Homstrom

                             Mama Askofu Mdegella akiwa na Mchungaji toka Chicago Marekani



Katibu Mkuu KKKT akiwa na Askofu wa Kusni Mashariki Askofu Mbedule mwenye miwani
 na Askofu Kinyunyu wa Dodoma
NI IBADA YA KILEE CHA JUBILII YA MIAKA 50 YA KKKT HAPA 
CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA
Madhabahu tayari kwa Ibada




                  Katibu Mkuu Bw. Brighton Kilewa akipokea zawadi ya KKKT toka Ujerumani


Askofu wa Ujerumani akisalimia na Askofu Mwakyolile
Maandamano yanaendelea hapa Makumira 










Mtoto akiwa na Mshumaa " Ishara ya Nuru na Iangaze"

                    WAZIRI MKUU MSTAAFU MH.FREDRICK SUMAYE  YUPO TAYARI


                                                                  Tayari kuingia Kanisani



Wenzi wa Maaskofu
SASA NI KUINGIA KANISANI TAYARI KWA IBADA

















































Matukio ya Jubilii katika picha 
                Mkuu KKKT Msataafu  akibadilishana mawazo na Askofu Mkuu wa Sweden
             Waliopta kuwa Maaskofu wa Dayosisi ya Kusini Kati (Makete) 
Wakiwa na Mkuu KKKT ni Askofu Dr. Solomon Swalo mwenye vazi jekundu,Askofu Manyewa mwenye vazi la zambarau na Askofu wa sasa Askofu Levis Sanga mwenye vazi jeupe



Wawakilishi wa BAKWATA -Arusha wakitoa Salam zao

Askofu wa Kanisa la Kilutheri  Kongo akitoa Salam

Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kilutheri Kenya akitoa Salam

Mkuu wa KKKT-Uganda akitoa salam

Katibu Mkuu wa Fungamano la Makanisa Duniani (LWF) akitoa salam
 Mchg. Junge


Hapa akitoa zawadi maalum


 Salam toka Makanisa na Vyama vya Kimisionari toka Ulaya na Amerika




                  Wawakilishi wa chama cha Lepzing Mission hapa Mchg. Kuger akitoa salam


Katibu wa Berlin Mision-Africa  Mchg. Dr. Reihard Kees



                              Wawakilishi wa Chama cha DAN Mission wakitoa salam


Askofu Mkuu wa kanisa la Sweeden

Katibu wa Chama cha Uamsho Sweden Mchg. Stephane Homstrom akitoa salam

Mwakilishi wa Unite Evangelical Mission (UEM)
Mchg. Mwombeki

Askofu wa Makanisa ya United Lutheran Church German


Wawakilishi wa Lapzing Mission -German

Wawakilishi wa Danish Mission

Wawakilishi wa Kanisa la Kilutheri Marekani



Askofu wa Kanisa la Kilutheri Canada

Sasa ni zamu ya WAASISI wa KKKT
                 



Askofu Mkuu Mstaafu Dr. Samson Mushemba akitoa salam kwa niaba ya Maaskofu Wastaafu


Maaskofu wastaafu na Wachungaji Wastaafu

                               Mjane wa  aliyekuwa Askofu Mkuu Dr.Sebastian Kolowa
Mjane wa  aliyekuwa Askofu Mkuu Dr.Sebastian Kolowa akitoa salam 
huku Mwenzi wa Mkuu KKKT  Mama Askofu Dr. Gehaz Malasusa akimsiliza 

                    Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akitoa Salam maalum za Jubilii
HITIMISHO LA JUBILII  YA  MIAKA 50

                                                      Waziri Mkuu akitoa salam za Jubilii 

Mkuu KKKT akitoa salam na itikio la salam za Waziri Mkuu


    Mkuu KKKT mstaafu akiwa Mkuu KKKT wa sasa hapa wanaelekea kuvua mavazi tayari kwa kupata chakula















 Askofu Kinyunyu wa Dayosisi ya Dodoma, Mkuu wa Jimbo la kaskazini KKKT-Iringa na Askofu Mbedule wa dayosisi ya Kusini Mashariki





Askofu Mstaafu  Mkuta wa Dayosisi ya Mara



 Katibu Mkuu wa Fungamano la Makanisa Duniani akiwa na Katibu Mkuu wa Ukanda wa Afrika


                          Mmiliki wa Blog hii  Mchungaji Kurwa Sadataley akiwa na viongozi hao





 SASA NI WAKATI WA CHAKULA









JUBILII KKKT YAFANA 

Huku Waziri Mkuu Mstaaafu Mh Fredrick Sumaye akilitaka Kanisa kuepuka na wanaotoa fedha kwa kutumia mgongo wa dini

Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dk Alex Malasusa (wa pili kulia) akiongoza ibada ya kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kwa kanisa hilo. Ibada hiyo ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Makumira, Arusha jana. Kushoto ni Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye. 
Arusha. Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amewataka viongozi wa dini na Watanzania kwa jumla kuwa makini na watu wanaojipitisha na kutoa fedha kutaka uongozi akisema hiyo imezaa matabaka kwa wanyonge kukosa haki za msingi kwa kuwa hawana fedha.
Sumaye alisema hayo jana kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), zilizofanyika Chuo Kikuu cha Makumira, Arumeru.
Mbele ya Maaskofu wote 20 wa Dayosisi zote za KKKT nchini na wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya nchi, Sumaye alisema jeuri ya fedha na mamlaka imesababisha mambo mengi machafu katika jamii ikiwamo wanyonge kukosa haki zao za msingi, huku wenye uwezo kifedha wakipata haki kwa kutoa hongo au rushwa.
Alisema hali imekuwa mbaya kiasi kwamba hata nafasi za uongozi hivi sasa zinapatikana pasi na kuzingatia uwezo kiutendaji na uadilifu wa mhusika na badala yake kinachoangaliwa ni mhusika anayeomba uongozi ametoa fedha kiasi gani za kuwahonga wapiga kura.
“Hata katika baadhi ya dayosisi na sharika zetu watu wamekuwa wakipewa sifa za ajabu si kwa sababu ya uadilifu wao au wema wao, bali kwa sababu tu wamechangia fedha kwa shughuli zetu za kanisa au hata binafsi,” alisema.
Aliwataka viongozi wa kidini kutojielekeza kwenye huduma za kiroho pekee, bali washughulike na mambo yote yanayoikwaza jamii wanayoiongoza ikiwamo kukemea vitendo viovu vinavyohatarisha usalama, amani na misingi ya Taifa.
Akizungumzia amani ya nchi, Sumaye aliwataka Watanzania kukemea vitendo viovu vinavyolikumba taifa bila kujali kama kukemea huko kutawaudhi wenye mamlaka na nguvu za fedha.
Alisema taifa litaangamia iwapo hali ya uhasama wa kiimani, kiitikadi na maeneo mabomu kutupwa kwenye mikusanyiko ya watu kwa nia ya kuua, itaachwa iendelee.
“Taifa linakabiliwa na matatizo mengi. Watu wamefikia hatua ya kuchukiana kwa sababu ya imani zao. Mabomu yanalipuliwa katika mikusanyiko ya jamii na kuteketeza watu wasio na hatia,” alisema Sumaye na kuongeza:
“Je, tumekuwa na ujasiri wa kukemea mabaya hata kama kukemea huko kunawaudhi au kuwakera wenye mamlaka au na wenye nguvu za fedha?”
Sumaye alihoji kilichotokea hadi leo Watanzania waanze kubaguana kwa maeneo wanakotoka, viongozi wa dini kuuawa, makanisa kuchomwa moto na Wakristo na Waislamu kupigana kugombea nani achinje mnyama.
“Haya yote ni mambo mageni nchini mwetu, tuendelee kuiombea nchi yetu amani lakini wakati maombi yakiendelea, Watanzania tujue tunajichimbia kaburi letu wenyewe kama hatutapiga vita maovu haya,” alisema.Sumaye aliyekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 ya Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, alihoji uadilifu na dhamira ya Watanzania, wakiwamo viongozi wa dini ambao hivi sasa wanawasifia na kuwakumbatia watu wanaotoa michango mikubwa ya fedha madhabahuni bila kujali uadilifu wao na jinsi walivyochuma fedha hizo.
Mkuu wa KKKT, Askofu Alex Malasusa alisema Kanisa halitaogopa kusema ukweli pale panapobidi huku akiahidi kuwa litaendelea kujenga marafiki wema bila kujali itikadi zao kisiasa wala ukwasi.
Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na viongozi wa Kiislamu kitendo ambacho Askofu Malasusa alisema ni ishara ya ushirikiano na uhusiano mwema kati ya dini na madhehebu yote nchini tofauti na chuki inayojaribu kupandikizwa na wasiolitakiwa mema taifa.
TUYAENZI YALE MEMA  YA KKKT
Hayo yamesemwa na Mchungaji Elisande Mhanga alipokuwa akihubiri katika kanisa lililopo ofisi Kuu za Dayosisi ya Iringa leo hii. Na alikuwa akikazia Mahubiri toka Mathayo 13:31-32
Pia Mchungaji Stephane Homstrom ambaye ni Katibu Mkuu wa  Chama cha Uamsho Swedeni-(Sweedish Evangelical Mission) kama kijulikanavyo kwa jina la SELM. Naye amesema ni bahati na ni Neema za Mungu tu kutufikisha hapa tulipo na tunapaswa kujipanga kwa ajili ya miaka hamsini (50) ijayo
                                                       Mchungaji Elisande  Mhanga
      Bw. Nayman  Chavalla
          Katibu Mkuu KKKT-Dayosisi ya Iringa akimkaribisha Mchungaji Stephan  Homstrom
 ili awasalimu watumishi wa Dayosisi katika Ibada ya leo hii hapa Chapel

                                                           Mchungaji Stephane Homstrom
                                              Katibu Mkuu wa  Chama cha Uamsho Swedeni


No comments

Post a Comment